Harmonize apigilia msumari kuhusu Diamond “Sina Mawasiliano na Diamond hatuongei hata kidogo”

MWASISI wa  Konde Worldwide, mwanamuziki Harmonize, amesema hivi sasa hana uhusiano wowote na bosi wake wa zamani wa kundi la Wasafi Classic, Diamond Platnumz, na kwamba hawawasiliani kwa njia yoyote.

“Namheshimu na anafanya kazi nzuri, lakini hatuna urafiki, kwa hili sitaki kudanganya. Tunaheshimiana, kwani tunatoka nchi moja ya Tanzania, lakini si marafiki.  Tulikuwa tukifanya kazi pamoja lakini sasa hatufanyi hivyo tena.  Hilo ndilo najaribu kulisema kwa sababu za kikazi,” alisema Harmonize.

Msanii huyo maarufu amenukuliwa pia na kampuni ya Mdundo ya Kenya akisema hana uhusiano wowote na wasanii wengine kutoka Wasafi tangu alipojitoa.

“Sitaki kusema uongo, mahusiano yangu na uongozi wangu uliopita siyo kama zamani, na kuhusu wao kushindwa kuhudhuria ndoa yangu, mimi niliweka nadhiri kuwa siku ya ndoa yangu ningependa wahudhuriaji wawe ni ndugu zangu nilioishi nao vizuri kijijini,” aliongeza.

Chini ya  Konde Worldwide, ameachia albam ya  ‘Afro East’  inayoshirikisha mastaa kadhaa wa Afrika kama Burna Boy.  Hivi karibuni, alishirikiana na wanamuziki Darassa, Country Boy, Young Lunya, Moni, Billnas, Rosa Ree, Baghdad katika ‘remix’ yake ya  ‘Bedroom’.

Pia amemchukua  Ibraah ambaye anaifanyia kazi EP ya kwanza kutoka Konde Music Worldwide ya Harmonize.  Wawili hao pia wanasemekana wako njiani kutoa kibao kipya kwa kushirikiana na mwanamuziki maarufu wa Kenya,  Otile Brown

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post