Mwanaume epuka kumwambia maneno haya mpenzi wako

Wanaume wengi hudhani ni vigumu sana kuwafurahisha wanawake lakini si hivyo, ni jambo rahisi, matendo yako kwenye mambo madogo madogo ya kimapenzi na kuchunga ulimi wako vinaweza kumfanya mwanamke wako kuwa na furaha kupita kiasi na kama yeye akiwa na furaha basi ndugu yangu maisha yako yatakua na amani na wewe utakua na furaha.

Kwa kawaida wanaume kuna vitu tunaviona vya kawaida sana na vya kipuuzi lakini kwa wanawake ni vitu muhimu na tunatakiwa kuwa makini tunapovizungumzia. Katika kukusaidia tu ndugu yangu katika mahusiano hapa nimekuandalia mambo matano ambayo unapaswa kuwa makini unapoyaongelea, hizi ni kauli tano ambazo mwanaume ni dhambi kabisa kumuambia mwanamke.

1. Hiyo Nguo imekutoa vizuri imefanya makalio yako yaonekane makubwa; Ingawa wanwake hupenda sana kusifiwa na kauli yako ilianza vizuri lakini umemalizia vibaya kumuambia ‘imefanya makalio yako yawe makubwa’ ni sawa na kumuambia umepigwa pasi na hata kama hatakujibu utamuumiza mbaya na kumuondolea kujiamini.

Sio kwamba alikuwa hajui kuwa makalio yake si ya mwendo kasi lakini kwa kumuambia wewe tena ukasema kapendeza kwasababu yanaonekana makubwa basi unamuambia kua unapenda makalio makubwa na kipindi chote hicho mlivyokuwa naye basi ulikua unavumilia tu na hufurahii. Ndugu yangu katika mahusiano achana na hiyo kauli, ishia tu kumuambia umependeza basi!

2. Kweli kabisa anza Diet; Hapa ni yeye kaja kukuambia kuwa anajihisi mnene na anataka kuanza diet ili apungue, ndugu yangu acha kujifanya kiherehere kuwa eti kweli anahitaji kupungua, hata kama unaona anahitaji kupungua mwanangu wewe sema tu unavutiwa hivyo hivyo na tena ukimshika shika kumuambia ndiyo unavyopenda mwili unakua na pakushika sio mifupa mitupu.

Akizidi kusisitiza wewe muambie hata kama anafanya hiyo diet basi asipungue sana. Hapo utakua umemuambia kuwa unampenda jinsi alivyo na unafurahia vile alivyo. Kumuambia kweli kabisa unatakiwa kufanya dieti ni sawa na kumuambia kuwa wewe ni mnene na siku nyingi nilitamani upungue sifurahii kabisa ulivyo. Kuwa makini na muonekano wa mwanamke, utamnyima raha na akikosa raha hutakuwa na raha.

3. Kwanini usiwe kama yule rafiki yako; Bila kujali unatolea mfano kitu gani lakini kamwe usimsifie rafiki yake na kumkosoa yeye hata kama ni kwa utani. Usiseme kwanini usingenunua rangi kama ya flani, au kwanini huwi mpole kama flani na mambo kama hayo, kutole amfano kuwa anatakiwa kua kama flani inamaana unampenda na kumfurahia flani kuliko yeye. Hata kama nia yako si hiyo lakini acha kumlinganisha na rafiki zake au wanawake wengine.

4. Kweli alipendeza…; Mmetoka out mlienda kwanye sherehe au sehemu na marafiki zake na wakati mnarudi au mko nyumbani anaanza kumsifia rafiki yake mmoja alivyokua kapendeza, ndugu yangu huo ni mtego usiongeze neno hata kama uliona kweli kapendeza. Kumuambia kweli alipendeza utakua umefanya makosa matatu, kosa la kwanza ulikuwa unamuangalia sana rafiki yake labda umemtamani ndiyo maana ulijua kapendeza.Kosa la pili umemuambia yeye hakupendeza kwani utakuwa labda ulimlinganisha na kosa la tatu hujali hisia zake unamuwaza huyo aloambiwa kapendeza. Msikilize tu na kama utachangia sema tu mbona kawaida tu hata hukuona kipya. Kwanini utafute matatizo ya bure muhimu ni usiponde sana kwani ukiponda zaidi atastuka unaongea vile ili kumfurahisha na si kweli, jibu kidogo kama vile hutaki na badilisha stori mara moja.

5. Hivi huwezi kunyamaza; Anaongea sana, analalamika sana lakini hupaswi kumuambia kua anaongea au kulalamika sana kwani utamfanya azidi kuongea sana na kulalamika kuwa unamuambia anaongea na kulalamika sana. Najua ushachanganyikiwa zaidi lakini ndivyo wanawake walivyo, hutoa stress zao kwa kuongea, ni njia ya kujitetea ni silaha ya mapambano kwao.

Kwa maana hiyo hata kama anaongea sana analalamika sana wewe umilia au jaribu kuzidi kumuonyesha mapenzi. Kulalamika kuwa anaonge ana kulalamika sana utampa kitu kingine cha kulalamika na utazidi kuchanganyikiwa zaidi kwani haitasaidia kumnyamazisha. Nikazi ya mwanaume kumpenda mwanamke bila kuuliza au kutaka kujua kwanini anampenda na wala usitake kumuelewa kwani kamwe hutamuelewa wewe mpende tu

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post