Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameliomba Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF iongezewe viingilio katika mechi zao kutokana na kiwango walichonacho.
Manara amesema hayo kutokana na mchezo wa jana wa ligi dhidi ya Kagera Sugar, ambao Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.
Manara amesema, "TFF na Bodi ya Ligi ongezeni viingilio katika mechi zetu, ni dhambi kulipa pesa ile kumuangalia Luis Miquissone akicheza.", amesema.
Aidha Manara amemzugumzia kiungo mpya wa klabu hiyo, Luis Miquissone kutokana na kiwango alichokionesha katika mchezo huo wa jana, "jana nilikuwa najiuliza namuangalia Messi au?", amesema.
"Sasa hivi kubaki nyumbani wakati Miquissone anacheza ni kosa linaloweza kukuweka 'lock up' wiki.", ameongeza.
Simba hivi sasa ina pointi 59 katika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 44 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Namungo FC yenye pointi 40 sawa na Yanga ambyo inakamata nafasi ya nne.
Tags
Michezo