Baba Kanumba na Mama Kanumba waingia tena Kwenye mgogoro mzito, amtuhumu Mama Kanumba kutaka kula mwenyewe mamilioni mengine ya Kanumba yanayotarajiwa kutolewa hivi karibuni na makampuni yaliyokuwa yakifanya kazi na Kanumba. Baba Kanumba anataka safari hii wagawane pasu kwa pasu sio mama Kanumba Kula mwenyewe Kama ilivyokuwa za awali -
Akizungumza na Globalpublishers kwa njia ya simu baba Kanumba alisema tayari ameshaweka pingamizi kuhusu fedha hizo asipewe mama Kanumba pekee kama zilivyokuwa zile za mwanzo bali wanawatakiwa wapewe wote kama wazazi.
“Mama Kanumba hakumpata Kanumba peke yake bali mimi kama baba nahitaji haki yangu na mimi, inakuwaje mama Kanumba amechukua zile fedha za mwanzo zilizotolewa na makampuni mbalimbali yaliyofanya kazi na Kanumba, amekula mwenyewe? Sasa sikubali,” alisema baba Kanumba. -
Baba Kanumba tayari ameweka pingamizi kuhusu pesa hizo ambalo limekubaliwa. Akizungumza na Amani, mdogo wa Kanumba, Mjanaeli Kanumba alisema fedha za Kanumba awamu ya pili zilitarajiwa kutoka hivi karibuni ambapo kutokana na pingamizi la baba yao bado hazijatoka. -
“Baada ya kuweka pingamizi, lilikubalika na baba aliitwa na Bodi ya Filamu afike Dar au atume mwakilishi kwenye kikao ambacho kingefanyika Februari 11, mwaka huu ambapo alinituma mimi nimwakilishe.
“Nilifika bodi ya filamu lakini cha kushangaza nikaambiwa kikao cha wajumbe wanaoshughulikia suala la fedha za Kanumba walikaa jana yake wakiwa na mama Kanumba na mama huyo kukubali kuwa atampa mgao mzee Kanumba lakini kidogo kama sadaka. -
“Baba kusikia hivyo akakataa na kushikilia kwamba lazima wagawane sawa na mama Kanumba maana ni vitu vingi vya Kanumba ametumia mwenyewe bila kumshirikisha,” alisema Mjanaeli.
Mjanaeli aliendelea kusema kuwa walikubaliana na watu wa bodi ya filamu kuwa kikao kijacho kitakachofanyika baada ya mtu anayehusika na fedha kwenye kampuni husika kurejea kutoka safarini watakuwepo pande zote mbili na hapo ndipo zitajulikana mbivu na mbichi. -
“Tunasubiri tuitwe kikao cha makubaliano kati ya mama na baba Kanumba ikishindikana tunapeleka kesi hii mahakamani,” alisema Majanaeli.
Tags
WASANII