Makubwa..Mke Aachika, Bintiye Aolewa na Mume Huyo Makubwa..Mke Aachika, Bintiye Aolewa na Mume Huyo

MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Grace, aliolewa zaidi ya miaka 18 iliyopita. Kama wanawake wengine, aliwaza kuwa na ndoa yenye amani na furaha, lakini ndoa yake iliharibika baada ya mumewe kumuoa mtoto wao wa kwanza.

Grace alipata manyanyaso mengi. Baada ya changamoto nyingi mumewe akauza mali na kumfukuza, na akajenga nyumba ya kukaa nyingine na kukaa na mkewe ambaye ni binti yao. Alipouliza kuhusu hilo, mwanaume huyo alijibu kuwa yuko huru kumuoa binti huyo kwa kuwa si binti wa kumzaa, ni binti wa kufikia.

Pia watu hao wamemfanya mtoto wa pili wa mama huyo amabye yuko kidato cha tatu kuwa teja kwa madawa waliyokuwa wanampa na kumtumia mtoto huyo kwenye kumfukuza mama yake. Kitu kilichofanya mama huyo aondoke ni kuwa kila jirani akifa mumewe huenda kulala na wajane hao, na akiulizwa humjibu kuwa ana wivu sana.

Mume huyo alikuwa na mahusiano na wajane na mara nyingine amekuwa akirudi na nguo au viatu vya waume zao ambazo mara nyingi vilikuwa havimtoshi.

Baadae aliona risiti za hospitali ndani mwao na akagundua kuwa mumewe anatumia ARVs, alipoulizwa alimwambia naye aanze kwenda kwa madaktari ili kupata vidonge vya kuzuia maambukizi ya ukimwi.  Alipopima na kuonekana hana maambukizi aliamua kuondoka na bintiye mziwanda ambaye baba huyo alijaribu kumbaka mara kadhaa lakini hakufanikiwa.

Aliondoka kwa mumewe na kuanzisha maisha yake lakini hayuko vizuri kiafya, anazimia mara kwa mara, lakini pia haja ndogo humtoka bila taarifa. Hali yake ya afya inamfanya asifunge mlango wake akilala, majirani zake humfungia ili likitokea lolote usiku waweze kumsaidia.
 Mtoto aliyemchukua wakati anaondoka alirudi kwa baba yake baada ya kutoridhika na hali ya maisha yao. Binti yake hivi sasa ana mtoto wa miaka mitatu, mtu ambaye anajua amezaa na mumewe.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post