Nahodha wa Simba, John Bocco leo ameongoza kikosi chake kushinda mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi.
Kipindi cha kwanza kilikamilika kwa Simba kuwa mbele kwa mabao 2-1 na waliongeza bao la tatu na mwisho dakika ya 53 kupitia kwa Ajibu akimalizia pasi ya Shiboub.
Sasa Simba inatinga hatua ya nusu fainali itamenyana na bingwa mtetezi Azam FC.
Tags
MAPINDUZI CUP