Bilionea
 namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amesema kuwa anatarajia 
kuinunua klabu ya Arsenal inayoshiriki Premier League ifikapo mwakani 
2021.
Nigerian billionaire Aliko Dangote has again declared his intention to buy Arsenal
Dangote
 ambaye ndiye tajiri namba moja barani afrika kwa mujibu wa jarida la 
Forbes anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola za Kimarekani 
bilioni 10.3 kupitia biashara zake.
Kwa muda 
mrefu bilionea huyo wa Nigeria amekuwa akihusishwa na kutaka kuichukua 
Arsenal ambayo inamilikiwa na Kroenke Sports & Entertainment (KSE).
Kunako
 mwaka 2018, Dangote aliwahi kuiambia Reuters kuwa “Tutaifuata Arsenal 
2020, hatakama kuna mtu atainunua, bado tutaifuata.”
Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 62, amekuwa akijihusisha na na miradi mbalimbali ya kibiashara ikiwemo saruji.
“Arsenal,
 ni timu ambayo nahitaji kuinunua siku moja, lakini ninachoweza kusema 
leo ni kwamba tuna dola bilioni 20 kama sehemu ya projekti na huko ndiko
 tunakotaka kujikita zaidi,” Dangote ameiambia David Rubenstein Show.
“Najaribu kumaliza ujenzi wa kampuni na baada ya kumaliza pengine mwaka 2021 tunaweza.” amesema Dangote.
“Siinunui
 Arsenal kwa muda huu. Nitainunua Arsenal wakati nitakapomaliza projekti
 zote kwa sababu nahitaji kuipeleka kampuni katika hatua nyingine.”
Tags
MICHEZO KIMATAIFA
