BIASHARA United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza kutoka mkoani Mara walibakiza dakika sita tu kuambulia pointi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga uliocchezwa uwanja wa Taifa ila bahati haikuwa yao walipoteza.
Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Tariq Seif dakika ya 84 akimalizia pasi ya nahodha Papy Tshishimbi akiwa ndani ya 18 na kuzamisha moja kwa moja wavuni.
Seif ambaye aliwahi kucheza Biashara United kabla ya kusajiliwa hivi karibuni kwenye dirisha dogo ndani ya Yanga akitokea nchini Misri amesema kuwa anaona fahari kuipa pointi tatu, timu yake.
"Nimefurahi kuona nimeipa ushindi timu yangu inaamanisha kwamba ninaweza na nitaendelea kupambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuwa bora zaidi," amesema.
Yangaimecheza jumla ya mechi 11 inafikisha jumla ya pointi 24 sawa na Kagera Sugar inakuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa ikiwa nyuma ya Simba walio kileleni wenye pointi 31 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 12
Tags
LIGI KUU TPL