VANESA AWABIPU BASATA, ATUPIA PICHA HIZI ZA UTUPU

Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ akiwa na mpenzi wake ambaye ni staa wa Marekani, Rotimi Akinosho. 

LICHA ya kwamba anaonekana anajiheshimu, msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amekwenda kinyume na alivyozoeleka na kuwabipu Basata baada ya kuachia video ya kimahaba akiwa na mpenzi wake ambaye ni staa wa Marekani, Rotimi Akinosho.

 

Vanessa aliweka video iliyokuwa ikiwaonesha wakiwa chumbani huku mwanadada huyo akiwa amevaa braa tu na mpenzi wake Rotimi akiwa kifua wazi ambapo alikuwa akimdekea kimahaba.

 

Baada ya kuweka video hiyo wafuasi wengi walionekana wakimshangaa kwani siyo kawaida yake huku wengine wakimpongeza na kumwambia aendelee kuwakomesha.

 

“Yaani Vanessa tangu awe kwenye mapenzi na Rotimi amebadilika sana siyo yule aliyekuwa akijiheshimu vile, kwa sasa anajiachia sana na hajali kabisa.



“Sasa hii video naona anawabipu Basata, wakiiona hapa lazima wamwite akajieleze maana mambo ya faragha anayaleta kwenye mtandao, siyo sawa kabisa,” aliandika mmoja wa wafuasi hao.

 

Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kumpata Vanessa ili aeleze sababu ya kuposti video hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, lakini simu yake haikupatikana hewani kwa kuwa yupo nchini Marekani kwa mpenzi wake huyo. Hata alipotafutwa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp hakujibu chochote

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post