Liverpool chini ya Kocha Mjerumani, Jurgen Klopp imeandika rekodi nyingine baada ya kushinda ubingwa wa dunia wa klabu.
Liverpool imebuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Flamengo ya Brazil katika mechi ya fainali kuwania klabu bingwa ya dunia iliyochezwa nchini Qatar.
Hadi dakika 90 zinamalizika, hakuna timu iliyokuwa imeona mlango wa mwenzake.
Dakika 30 za nyongeza, Roberto Firmino raia wa Brazil, aliimalizia kazi nzuri ya Sadio Mane kufunga bao safi dhidi ya Wabrazil wenzake.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA