Ukitazama angani kuna vitu vingi utaona lakini kuna kitu kimoja tu ambacho ndicho hubadili nyakati na majira. Kuna wakati kitu hicho hupata upinzani na ukizani mkubwa
Mara utasikia kupatwa kwa jua, Mara kupatwa kwa mwezi, Mara dalili ya mvua ni mawingu.
Mawingu yakitanda sana basi kitu hicho hukosa nguvu japo husubiri mawingu yaondoke ili kiendelee na kazi yake. Kitu hicho hakina mbadala, Ni hicho pekee kazi yake haina msaidizi. Kitu hicho ni JUA ambalo kwa jina lingine huitwa mfalme wa Anga. Mawingu yanapopishana na kukimbia ndipo nyakati hubadilika na duniani tunapata matumaini ya kupata mwanga tena.
Mwanamke ni kama jua kwa mumewe
Mwanamke huangaza familia kusababisha mafanikio makubwa pale anapokuwa na furaha. Lakini anapokutana na upinzani na ukinzani hukosa furaha na mimea ya baraka kushindwa kuchipua katika familia kama ambavyo jua lisipoangaza dunia hakuna mmea uta survive.
NISIKILIZE MWANAUME
Japo wanasema "Chozi haliachi doa" lakini chozi la mwanamke huacha doa kubwa.
Japo wanasema kitanda hakizai haramu lakini ukimsaliti mkeo utaona utakavyo zaa haramu kwelikweli.
Hesabu hazidanganyi
1+1=2 tofauti kabisa na 1×1=1
Mungu ndiye kielelezo cha mahusiano
Kama ambavyo mwanaume ndiye mwazilishi wa ndoa. Mungu anakupenda mwanadamu japo unakosea sana, Mungu anasamehe hata bila kuombwa msamaha, Anatenda mema hata kwa watu wanaomtukana vibaya.
Mwanamke amekuzalia, amekupa heshima, anakutunzia familia, amewaepuka wengine yuko na wewe, anafanya mengi kwa ajili yako kwanini uhesabu machache aliyokukosea na kumchukia?. Chozi la huyo dada halitakuacha salama.
Kifupi
Mwanamke akikushinda ujue mwanaume huna upendo pia huna akili. Maana biblia imesema wapendeni wake zenu kama kristo alivyolipenda kanisa, Ishini na wake zenu kwa akili.
Ukihitaji baraka na mafanikio katika maisha yako, Kwanza itulize ndoa yako, usiruhusu migongano, Jua likiangaza katika nchi, mimea humea sana na shughuli za binadamu hufanyika.
Lakini giza likitanda mimea huangamia na shughuli za binadamu husimama. Basi mwanamke akicheka ndani ya familia yako ndipo mafanikio yataandamana kwako. Mwanamke akilia utapokea kila aina ya matatizo hivyo kuwa makini na kulia kwa mwanamke

Tags
MAHUSIANO