Aliyekuwa kiungo wa Simba kwa msimu uliopita, Haruna Niyonzima ametamka kwa mdomo wake kwamba anakuja Yanga na amewataka mashabiki wakae mkao wa kufurahi. Kiungo huyo mchezeshaji aliyewahi kukipiga Yanga na Simba, sasa ni nahodha wa AS Kigali ya Rwanda.
Niyonzima amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa tulieni nakuja mapema tu. Mnyarwanda huyo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachowavaa watani wao Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Januari 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Niyonzima alisema: “Yanga niliondoka msimu wa 2016/17, baada ya mkataba wangu kumalizika na nilishindwa kufi kia makubaliano mazuri ya kuongeza mkataba mwingine kabla ya kuamua kwenda kusaini Simba.
“Nafahamu wakati ninaondoka mashabiki wa Yanga hawakupenda, lakini maslahi ndiyo yaliyoniondoa siyo kingine lakini nilikwenda huko sikuwa na upepo nao mzuri na ndiyo maana mkataba wangu ulivyoisha niliamua kuondoka zangu.
“Lakini ninarejea tena Yanga ikiwa ni klabu iliyonilea, kunikuza na kunifi kisha hapa nilipo, hivyo ninakuja kwenye timu ninayoipenda, ninaahidi kuipambania kwa kipindi chote nitakachokuwepo hapo,” alisema Niyonzima maarufu kama Fabregas. Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla hivi karibuni alithibitisha kumsajili kiungo huyo mwenye ufundi mwingi mguuni
Tags
Michezo