Kocha Mwinyi Zahera katika mahojiano na Clouds FM katika kipindi cha SporsXtra amenukuliwa akisema “Pesa ambazo nilikuwa nazitoa Yanga nilikuwa nafanya hivyo kwa kusaidia hakuna siku nimetoa pesa nikadai wanirudishie. Tangu nimefika Yanga nimesaidia pesa ambayo inaweza kufika hata dola ($) 50,000 (zaidi ya Tsh. milioni 100). Kuna wakati wachezaji walikuwa wananifata wanaomba niwaazime pesa halafu watanirudishia wakilipwa mishahara yao.”
Tags
Michezo