Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, S2Kizzy ambaye ndiye aliyefanya ngoma ya ‘Baba Lao’ amefunguka kuhusu ku-copy ngoma ya ‘Soapy’ ya Naira Marley kwa kusema kuwa walikuwa ‘inspired’ na ngoma hiyo.
Akijibu tuhuma hizo kwenye mahojiano yake na Wasafi FM, S2Kizzy amesema kuwa yeye na Diamond walianza kutengeneza wimbo wa ‘Baba Lao’ muda mrefu sana na hadi kutumia wimbo huo wamepata ruhusa kutoka kwa Naira.
“Kitu ambacho watu hawajui kuhusu ngoma ya ‘Baba lao’ ni kwamba tulianza kurekodi kitambo sana, Wakati tukiwa Madagascar mimi Diamond. Tulienda na studio ndogo siunajua sisi ni watu wa muziki tukawa tunagonga mawe tu. Tulikuwa tumekaa tunagonga ngoma fulani slow hivi.” amesema S2Kizzy na kueleza walivyovutiwa na ngoma ya Soapy.
“Pale tulipokuwa tumekaa palikuwa na TV inaonesha chaneli fulani hivi, mara ikapita ngoma fulani ya Naira Marley ‘Soapy’ tukasema mbona kama ngoma ina vibe fulani hivi..Na siku tunaweza kufanya ngoma kama hii. Basi tukaona ngoja tufanye ngoma kama hii halafu tutawasiliana nao wenyewe. Kwa hiyo tukawa inspired na wimbo wa Naira Marley unaitwa ‘Soapy’, Kwa tukaona tunaweza tukaweka maneno yetu, Vibe letu na vitu vyetu lakini kwenye type ya muziki kama huo.” amesema S2Kizzy.
Kwa upande mwingine, S2Kizzy amesema kuwa Diamond ni msanii mkubwa Duniani hivyo hawezi kutumia wimbo wa mtu yeyote bila ruhusa, Na hata kutumia vionjo vya ngoma ya ‘Soapy’ amefanya mawasiliano na Naira Marley.
Tags
WASANII