ILIPOISHIA
“Kuna nini?”
Xaviela akajikaza kuliiza swali.
“Yul…e yule jaji wenu aliye kuwapo hapa. Tumemkuta amenyongwa hadi kufa ndani ya gari lake”
“Nini?”
Xaviela aliuliza kwa mshangao. Kwani habari hiyo imezidi kuwatia machungu zaidi, kwani kufungwa kwa akaunti zao na kufa kwa huyo jaji Josephati waliye kuwa wana mtegemea kwenye kuweka pingamizi katika ndoa ya baba yako na Olvia Hitler, kumemaliza kabisa ndoto za wao kupinga ndoa ya baba yao na Olvia Hitler.
ENDELEA
Xaviela na Frank wakakimbilia katika eneo la tukio huku wakimuacha Xaviena akishindwa hata kusimama hii ni kutokana kunyong’onyezwa na mambo hayo mawili yaliyo tokea kwa muda mfupi sana kwake. Frank na Xaviela wakakuta jaji Josephat akipakizwa kwenye machela na kupelekwa katika chumba cha cha matibu kwa ajili ya kupimwa ni nikitu gani kimetokea, kisha ripoti hiyo iweze kuwafikia polisi.
“Amekufaje kufaje sasa?”
Xaviela alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Nilimkuta ndani ya gari lake akiwa amelala na inavyo onekana mtu aliye mnyonga ni professional kwa maana milango yote ya gari ime fungwa kwa ndani na mtu akiwa kwa nje hawezi kufungua”
Frank alizungumza huku wakilitazama gari la jaji Josephat. Xaviela akaka kimya huku akiwaza hali halisi ya mauajia hayo.
“Kuna kitu hapa ambacho sio cha kawaida”
“Kitu gani?”
“Sijui ila kuna jambo ambalo lina endelea”
“Kwa nani sasa lina endelea hilo jambo?”
“Sijajua Frank ila kuna jambo linalo endelea”
Majibu ya uchunguzi wa daktari yakaonyesha shingo ya jaji Josephat imevunjwa hadi kupelekea umauti wake. Ila kila walipo jaribu kutafuta alama za vidole kwenye shingo hiyo hawakuweza kuzipata jambo ambalo likazidi kuwawia ugumu askari juu ya wapi waanze kufanya upelelezi wao.
Xaivena aliye shindwa kwenda kushuhudia mambo yote hayo, akaitafuta namba ya baba yake na kumpigia, simu ya baba yake ikaanza kuita na kupokelewa.
“Baba”
Xaviena alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Baba una nisikia?”
Xaviena aliendelea kuzungumza ila baba yake hakuweza kuzungumza chochote. Simu ikakatwa, Xaviena akapiga tena simu ya baba yake na kukuta ikiwa imezimwa kabisa.
***
Eddy mara baada ya kuzima simu yake ili kuepuka usumbufu wa watoto wake, akarudi chumbani alipo muacha Olvia Hitler mara baada ya kurudi kutoka katika kituo cha kulelea watoto yatima.
“Eddy”
“Niambie mume wangu”
“Nimepokea meseji kutoka kwenye ile kampuni kwamba walinzi wapo tayari kwa ajili ya kuletwa hapa nyumbani”
“Sasa si hatujawalipa”
“Usijali nimesha lipa mwaka mzima. Hivyo hakuna wasiwasi wa aina yoyote, jambo la msingi kwa sasa ni kuhakikisha kwamba ulinzi wa hii nyumba una kuwa ni mzuri. Pia nitaajiri walinzi binafsi wane waweze kukulinda”
“Nashukuru sana mpenzi wangu”
“Usijali mume wangu. Pia nitakuandalia timu ya kuhakikisha kwamba inaandaa kampenzi zako za ubunge kwa maana uchaguzi umebaki mwezi mmoja na nusu kabla ya kuanza”
“Nimekuelewa mke wangu. Ehee kwenye ndoa yetu una hitaji tuvae nini?”
“Chochote mume wangu”
“Sawa mke wangu”
Eddy na Olvia Hitler wakachagua mavazi ya kuvaa siku ya harusi yao ambayo ni siku mbili zijazo mbele.
***
“Siwezi kurudi na kumsujudia baba”
Xaviela alimuambia Xaviena aliye pendekeza wazo la kurudi nyumbani kwa ajili ya kumshawishi baba yao aweze kuwafungulia akaunti zao.
“Ila Xaviela, sisi tutaishije pasipo pesa?”
“Nitafanya chochote kuhakikisha nina endesha haya maisha yetu.Hakuna haja ya kumshobokea mtu ambaye hana shobo na sisi”
“Ahaa samahani daktari ana waita”
Nesi mmoja alikatisha mazungumzo ya Xaviena na Xaviela.
“Wapi?”
“Nifwateni”
Xaviela na Xaviena wakaongozana na nesi huyo hadi katika ofisi ya daktari. Wakakaribishwa na dokta Massawe ambaye ni miongoni mwa madaktari walio mfanyia upasuaji mama yao.
“Kwanza poleni sana kwa hali ya mama”
Dokta Massawe alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama Xaviana na Xaviela.
“Tunashukuru dokta, hali ya mama ina endeleaje?”
“Sio vizuri sana. Leo asubuhi tumekaa jopo zima la madaktari tulio mfanyia upasuaji mama yako. Tumeshauriana kwa pamoja mama yako aweze kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi. Kuendelea kukaa hapa hospitalini, ina weza kumchukua muda mrefu sana kwa yeye kuweza kupona na mukizingatia hapa hospitalini hakuna vifaa vingi sana.”
Habari hii kidogo ikaanza kuwapa mawazo mazito Xaviela na Xaviena.
“Ahaa........sasa sisi huko India tuna jua ni hospitali gani ambayo mama yeyu ana weza kutibiwa na akapona kabisa”
“Ipo hospitali ambayo tuna ubia nao. Hospitali hiyo ina shuhulika na kila ugonjwa. Tuna imani kwamba mama yetu ata patiwa huduma nzuri sana na atapona”
“Garama za kwenda huko ni kiasi gani?”
“Garama za awali zinaweza kufika hadi dola laki moja na nusu.”
“Ohoo Mungu wangu”
Xaviena alizungumza huku akionekana kukata tamaa.
“Mbona muna stuka. Vipi kwani mzee hana kiasi hicho cha pesa?”
Xaviena na Xaviela wakatazamana.
“Anazo”
Xaviena aka jibu kwa unyonge sana hadi daktari akaanza kuhisi kuna jambo linalo endelea kwenye familia hiyo ambayo nimaarufu sana katika mkoa wa Tanga.
“Basi ina bidi mumpatie taarifa ya nini kinacho takiwa kufanywa na ikiwezekana ndani ya wiki hii mgonjwa aweze kupelekwa India”
“Sawa”
“Ila mbona baba hajafika hapa hospitalini?”
“Ahaa…ha…”
Xaviena alizungumza huku akiwa ameshikwa na kigugumizi.
“Ukweli ni kwamba baba yetu kwa sasa hatupo pamoja naye kwenye maswala mazima ya uuguzi. Dokta wewe ni mtu mzima na una weza kutusaidia katika hili. Baba yetu ana pesa nyingi sana na hata sisi wenyewe tuna pesa nyingi sana ila baba amezifungia akaunti zetu ndio maana unaweza kuona tumeshangaa kwa kiasi hicho chapesa hatuna kwa sasa”
Xaviela alizungumza kwa ujasiri na kumfanya dokta huyo kujawa na mshangao.
“Baba ana mahusianona mwanamke mwengine ndio maana muna muona hapa hayupo na wala musitarajie kumuona”
“Xaviela”
“Nini, nina ongea ukweli. Dokta dola laki moja na nusu hatuna. Huyu mdogo wangu usiku wa kuamkia leo ameingiziwa dola milioni moja na kwenye akaunti yake ila asubuhi ya leo zime fungwa hizo akaunti, kwa hiyo hatuna pesa. Labda tutafute hicho kiasi na sidhani kama tuta kipata ndani ya siku mbili hizi”
Xaviela alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama daktari huyo usoni mwake.
“Naombeni namba ya baba yenu”
“Sawa”
Xaviena akamtajia daktari huyo namba ya baba yao. Dokta akapiga namba hiyo huku akiweka loud speaker.
“Habari”
Daktari alizungumza mara baada ya simu hiyo kupokelewa.
“Una hitaji nini”
Sauti ya Olvia Hitler ikawastua sana Xaviela na Xaviena, hata daktari mwenyewe akastuka.
“Aha…samahani naweza kuzungumza na muheshimiwa”
“Sikia wewe dokta, sihitaji umsumbue mume wangu. Kama ni swala la mapenzi na huyu mfu mtarajiwa huko hospitalini walisha malizana.”
“Olvia kwa nini unaongea hivyo?”
Xaviena alizungumza kwa suati ya upole huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Xaviena”
“Kwa nini una muita mama yangu mfu mtarajiwa. Ulikuwa rafiki yangu ili kuniumiza eheee?”
Xaviena alizungumza kwa unyonge sana na sauti iliyo maumivu.
“Sio hivyo Xaviena. Niambie ni kitu gani una hitaji”
“Naomba umuache baba yangu. Namuomba baba yangu arudi mikononi mwa mama”
“Baba yako mimi sikumuita. Baba yako alinipenda yeye mwenyewe na hata nilipo mshauri juu ya swala la familia yake, ila hakunipa jibu zuri zaidi ya kunijibu vile anavyo jisikia”
“Olvia mama yangu ana kufa. Hatuna pesa baba amefunga akaunti zetu. Tunahitaji pesa ya kumtibu mama yetu”
Xaviena aliendelea kumnyenyekea Olvia Hiler kwani bila ya kufanya hivyo hawato wea kupata msaada wowote kutoka kwa baba yao.
“Xaviena unajua jinsi gani ninavyo kupenda. Wewe pekee ndio ninaye kusikiliza. Nakuomba unikubalie jambo moja”
“Jambo gani Olvia”
“Naomba uniachie baba yako na yeye aiachie akaunti yako ya benki. Ukifanya hivyo mimi nitakuwa na amani. Usiingilie mapenzi ya baba yenu, kwani kupitia wewe ndio maana hadi leo mama yenu ana pumua, ila nawe ukienenda kinyume na mimi, hatuto zungumza kwa upole kama hivi. Umenielewa Xaviena”
“Sawa nimekuelewa Xaviena.”
“Basi nitamuambia baba yenu sasa hivi aweze kufungua akaunti yako tu”
“Nashukuru”
Simu ikakatwa na dokta akabaki akiwa amejawa na mshangao.
“Huyu mwanamke ni nani haswala hadi amezishika akili za baba yenu namna hiyo?”
“Anaitwa Olvia Hitler, alikuwa ni mpenzi wa zamani wa baba, ila mama aliweza kushinda katika vita ya kuishi na baba hivyo kwa kipindi chote mama aliishi nasi sasa Olvia Hitler na ameamua kumchukua baba yetu”
Xaviela alizungumza kwa upole huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Mmmm hilo ni jambo kubwa sana ambalo muda ndio una weza kuliamua. Ila kama mulivyo msikia huyo mwanamke tafadhali musiingilie hiyo vita. Nyinyi ni watoto, jambo kubwa ni kuhakikisha kwamba mama yenu ana rudi kwenye hali yake ya kawaida. Kisha hayo maswala ya mapenzi yeye ndio atakuwa muamuzi wa mwisho.”
Dokta Massawe alizungumza na kuwafanya Xaviena na Xaviela kukubaliana na ushauri huo. Ujumbe mfupi wa meseji ukaingia kwenye simu ya Xaviena. Akausoma na ujikuta akitabasamu, kwani amepata meseji kutoka benki inayo mueleza kwamba kwa sasa ana weza kutumia akauti yake hiyo ya pesa.
“Vipi?”
“Naweza kuitumia sasa akaunti yangu”
“Basi, inabidi tuandae utaratibu safari hata ikiwezekana leo usiku mama awe kwenye ndege”
Xaviela alizungumza huku akiwa amejawa na matumaini ya kuhakikisha kwamba mama yao ana kuwa katika hali salama. Kwa kushirikiana na dokta Massawe wakaanza kufanya utaratibu wa safari na kwa bahati nzuri wakapata ndege inayo elekea nchini India siku inayo fwata na itaondoka jiji la Dar es Salaam majira ya saa sita mchana.
Xaviena na Xaviela wakakubaliana mmoja wao aweze kwenda nchini India huku Xaviena akitakiwa kujiunga kwenye kampeni ya shirika la Cocacola kwa ajili ya kutangaza biasara ya kampuni hiyo.
Siku hiyo wakakodi ndege ndogo na wakaondoka Tanga kuelekea jijini Dar es Salaama huku wakiwa wameongozana na madaktari wawili walio tolewa na hospitali kwa ajili ya kumuangalia Rahma katika safari hiyo ndefu ya kuelekea nchini India.
“Xaviela hakikisha kwamba mama ana kuwa salama. Nina kuamini sana dada yangu”
Xaviena alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Sawa mdogo wangu nita hakikinsha mama ana kuwa salama na atapona.”
Kiasi cha dola laki nne alicho kiingiza Xaviena kwenye akaunti mpya ya dada yake, kitatumika katika maswala yote ya matibabu.
“Jichunge na wewe. Hakikisha moyo wako haumpi mwanaume yoyote”
“Nimekuelewa dada yangu”
Xaviela, Xaviena, madaktari na Rahma ambaye hadi sasa hajitambui, wakaka hapo uwanja wa ndege hadi siku iliyo fwata. Majira ya saa sita Rahma akaingizwa kwenye ndege hiyo ya fly emirates na kuwekwa kwenye daraja la V.I.P.
Ikawa ni wakati mwengine mgumu wa Xaviena na Xaviela kutengena. Kila mmoja alijikuta akiangua kilio, ila hapakuwa na jinsi ni lazima watengane ili kuhakikisha kwamba mambo yote wanayo yapigani kwenye maisha yao haya mapya ya kuishi pasipo kuwa na baba yana timia. Xaviela akaingia kwenye ndege na kumucha Xaviela peke yake uwanja huo wa ndege. Xaviela akaelekea eneo alipo mama yake na madaktari na kukaa kwenye siti yake huku mama yake akiwa amelazwa kwenye kitanda kilicho zungukwa na mashine zinazo msaidia katika kuhema.
‘Olvia utalipa kwa haya yote yanayo tokewa kwenye familia yangu’
Xaviela alizungumza huku akimtazama mama yake aliye alala huku hajitambui kabisa. Xaviena akaka uwanja huo wa ndege hadi ilipo ondoka na kupotea kabisa kwenye uwepo wa macho yake. Gafla Xaviena akastuka mara baada ya kuguswa begani mwake. Akageuka nyuma kwa haraka, hakuamini kumuona Olvia Hitler eneo hilo, tena akiwa na baba yake na wote wawili wana tabasamu kwa kejeli.
ITAENDELEA
Install Application ya Ufundi Kitandani tu Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi