Benzema sasa ni Moto


Straika wa Real Madrid, Karim Benzema sasa yupo vizuri katika timu yake kutokana na kufunga mabao mengi.

Mchezaji huyo yupo katika ubora wa juu kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Real Madrid mwaka 2009, ametupia mabao 17 msimu huu huku akiwa amepiga mashuti 47.

"Ninawapa pole sana wale wanaoanza kuuona sasa ubora wa Karim Benzema,” alisema Solari wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.

Benzema anafanya vizuri msimu huu tofauti kubwa na alivyokuwa katika msimu uliopita. alifunga mabao mawili wakati Real Madrid ilipoichapa Girona 3-1, Alhamisi iliyopita kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali ya Copa del Rey.

Kushuka kiwango cha Benzema katika miaka ya karibuni kulifanya watu waanze kufikiria hatakuwa na muda mrefu Real Madrid.

Hata hivyo, amerudisha makali yake katika kipindi timu yake inasaka mtu wa kufunga mabao kufuatia pigo la kuondokewa na Cristiano Ronaldo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post