Poshi: Situmii Mwili Wangu Kutafutia Fedha

Poshi: Situmii Mwili Wangu Kutafutia Fedha
MREMBO Queen Obed ‘Posh Queen’ amefunguka kuwa haamini kuutumia mwili wake kama biashara ili aweze kujipatia fedha kama ambavyo wanavyofanya warembo wengine kwa sababu hata Mungu hapendi. Akizungumza na Ijumaa, Posh alisema mwili na umbo zuri amepewa kama zawadi kutoka kwa Mungu hivyo hawezi kuutumia vibaya kwani atakuwa anamkosea aliyempa.

“Kuna watu wengi wananisumbua sana wakijua mimi ni kama wale, hapana, kiukweli ninajiheshimu na watu wanaonifikiria kuwa najiuza hivyo nawaambia kuwa hapa siyo mahali pake kabisa, nimeitafuta elimu ili niweze kupata kazi ya kujikimu maisha yangu mwenyewe,” alisema Posh

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post