Wema Sepetu afikishwa Mahakamani


Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili ya kusambaza picha zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii.




Oktoba 26, Bodi ya Filamu nchini, ilitangaza kumfungia muigizaji huyo kutojishughulisha na uigizaji kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake hizo zilizosambaa mtandaoni.
Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB),  Joyce Fissoo alisema kuwa Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni licha ya kuonywa na vyombo husika mara kwa mara.
"Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii,  na kwakuwa amekwisha onywa mara kadhaa safari hii tumeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu", amesema Fissoo.
Mapema Oktoba 26, kabla ya uamuzi wa huo, Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambapo ilimuonesha akiwa faragha na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.
Endelea kufuatilia www.eatv.tv, kwa taarifa zaidi kuhusiana na yatakayojiri mahakamani.
 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post