Mahadhi wa Yanga afanyiwa upasuaji mara mbili


Juma Mahadhi amefanyiwa upasuaji kwa mara ya pili baada ya ile ya awali kukosewa, hivyo atakuwa nje kwa wiki tatu.

Awali, nyota huyo aliumia goti mapema hata kabla ya  Ligi Kuu ya Bara kuanza na kufanyiwa upasuaji ambao ulimuweka nje na baadaye imebainika alikosewa.

Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema nyota huyo ameongezewa muda wa kukaa nje baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.

“Mahadhi kwa sasa ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu sababu awali alifanyiwa upasuaji wa goti lake lakini walikosea, hivyo wamemrudia kumfanyia upasuaji.

“Kurejea uwanjani pia itategemea na ripoti ya daktari wake,” alisema Hafidhi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post