Nick Minaji Amblock Cardi B Kisa Hiki Hapa

Nick Minaji Amblock Cardi B
SI unakumbuka kale ka msemo ka mafahari wawili hawakai zizi moja? Basi unaambiwa siku chache baada ya staa wa kike wa Hip Hop kutoka Marekani, Cardi B kumfuata ‘dairekti meseji ya Twitter’ (DM) na kumpa vitisho rapa Nick Minaj, inaelezwa Minaj amemaindi kinoma noma na kuamua ‘kumblock’ kila kona.

Ishu yenyewe ilikuwa hivi; Cardi B aliingia DM kwenye ukurasa wa Nicki wa Twitter na kutoa boonge la ‘biti’ lisilokuwa na ‘kichwa wala miguu’ ambapo sasa, kwa upande wa Nicki alimaindi hivyo akachukua hatua ya kumblock ili isiwe tabu.

Mmoja wa mashosti wa Nicki aliuambia Mtandao wa MTO (Media Take Out) kuwa, Cardi B amekuwa na tabia ya ukorofi f’lan hivi ambapo si Nicki peke unaomkera bali hata mastaa wenzake wengi.“Nicki hakupenda kugombana na Cardi B na ndio maana akaamua kumpiga block ya maana kwenye mitandao yake yote kijamii,” alisema shosti huyo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post