Adhabu aliyopewa meneja wa Simba SC kwa kuhujumu Taifa Stars

Kamati ya maadili ya sirikisho la sola Tanzania TFF leo Jumatatu ya September 10 2018 imefanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza adhabu kwa meneja wa Simba Robert Richard.
TFF leo imetangaza kumfungia mwaka mmoja kujihusisha na maswala ya soka Robert Richard na faini ya Tsh milioni 4 kwa kamati ya maadili kumkuta na hatia ya makosa mawili kuihujumu Taifa Stars kwa kutotii maagizo ya TFF na kuchelewesha wachezaji Simba SC kufika kambi ya Taifa Stars.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri wachezaji sita wa Simba SC John Bocco, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Shomary Kapombe na Erasto Nyoni waliachwa Taifa Stars na kocha mkuu Emmanuel Amunike kwa kushindwa kufika kwa wakati.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post