Maamuzi ya TFF kwa viongozi wa Simba baada ya kuwaondoa wachezaji wao Taifa Stars


Shirikisho la soka Tanzania TFF baada ya kuwaondoa wachezaji sita wa Simba SCkatika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa madai ya utovu wa nidhamu wa kutofika kambini katika muda waliopangiwa August 29 2018.

TFF sasa wametangaza pia maamuzi mapya kwa viongozi wa club hizo kutokana na kushindwa kuhakikisha wachezaji wao, wanafika kambini kwa wakati, TFF imetoa taarifa kuwa viongozi wa Simba kaimu katibu mkuu wao Hamis Kisiwa na meneja wa timu hiyo Richard Robert watafikishwa katika kamati ya maadili ya TFF kwa kushindwa kufuata maagizo halali ya TFF ya kuhakikisha wachezaji hao wanajiunga na timu ya taifa.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa StarsEmmanuel Amunike amewaondoa wachezaji sita wa Simba SC katika list yake ya wachezaji wanaojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda September 8 2018 kwa kushindwa kuwasili kambini katika muda aliokuwa amepanga bila sababu za msingi, wachezaji waliondolewa ni John Bocco, Erasto Nyoni,Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, Jonas Mkudena Shomari Kapombe wakati Aishi Manulaakisalia katika kikosi cha Taifa Stars kwa kufika kambini kwa wakati.

Kitu Mzee Akilimali kaongea kuhusu stori za Yussuf Manji kurudi Yanga SC

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post