Diamond na Bob Junior Wamaliza Tofauti Waandaa Kazi ya Pamoja


C.E.O wa WCB Wasafi Diamond Platnumz wamekutana na aliyekuwa producer wake wa hits songs mbalimbali za Diamond kipindi cha nyuma Bob Junior.

Bob Junior ni msanii wa bongofleva na pia producer wa kwanza ambaye ndio alirekodi Album ya kwanza ya Diamond Platnumz enzi hizo ikiongozwa na hits kama Kamwambie na Mbagala, baadae waligombana na kukaa bila kuzungumza kwa miaka ingawa Diamond alitaka amani na akataka suluhu na Bob, japo ilifanikiwa wakakutana mpango wa Diamond haukufanikiwa

Wasanii hao wawili walikuwa na tofauti kipindi cha katikati kwani maelewano yao hayakuwa mazuri kutokana na kutofautiana kikazi,lakini sasa hivi wako sawa kwani Bon Junior amepost video kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na Diamond akikaririwa akisema “kuna kitu kikubwa kinakuja”

Diamond na Bob Junior waliingia kwenye ugonvi kupitia sababu nyingi sana wengine wakisema eti wanagombania Jina la Sharobaro wengi jina la Wasafi huku wengine wakienda mbali zaidi wakisema Diamond aliwahi kumwalika Bob katika moja ya sherehe na Bob aligoma kwenda ndipo bifu lao lilipoanzia.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post