WANACHAMA YANGA WATAKA MKUTANO MKUU UITISHWE HARAKA


Baada ya viongozi wa juu kadhaa Yanga kuachia ngazi, wanachama wengi wa klabu hiyo wameutaka uongozi uliopo kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura.

Hatua hiyo imefika kutokana na nafasi za viongozi waliojizulu kuachia nafasi zao na sasa kumebaki patupu ikiwemo ya Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa klabu na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwanasheria na mdau wa Yanga, Frank Chacha, amesikika akisema ni wakati mwafaka wa Yanga kuitisha mkutano huo kuweza kujadili namna gani ya kutafuta mbadala wa walioachia ngazi.

Chacha ameeleza kuwa ni muda mwafaka kufanya hivyo kwasababu baadhi ya mambo hayatakuwa yaanenda sawia ndani ya klabu hivyo ni vema mkutano ukafanyika.

"Mimi naona Yanga ni vema wakaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya kujadili mchakato mzima wa kuwapata viongozi watakaochukua nafasi za waliojizulu. Klabu haiwezi kwenda sawa bila ya viongozi" alisema.


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post