PICHA: Mbeya City wamezindua jezi zao mpya 2018/19


Kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2018/2019, club ya Mbeya City ya jijini Mbeya leo imezindua rasmi jezi zao mpya watakazozitumikia katika michezo ya Ligi Kuu na Kombe la FA msimu wa 2018/2019.
Mbeya City leo imeweka rekodi ya kuwa club ya kwanza Tanzania kutangaza au kuzindua jezi aina mbili tofauti ambapo kutakuwa na jezi za nyumbani na ugenini zitakazotumika kwenye Ligi Kuu pekee na zitakuwepo nyingine zitakazotumika katika Kombe la FA pekee.
Jezi za Mbeya City msimu huu zimetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Sports Masters ambayo imekuwa ikiwadhamini kwa msimu wa pili sasa, meneja wa Sports Master Fadhili Nsemwa amethibitisha kuwa wamefanya hivyo ili kuboresha na kuleta mabadiliko.
“Kila mwaka tunakuja na kitu kipya Mbeya City inakuwa club ya kwanza nchini kuwa na jezi maalum ya Kombe la FA pamoja na sare za makocha na msemaji wa timu”>>> Fadhili Nsemwa

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post