Millioni 70 kumng'oa Kessy Yanga


Imeripotikuwa kuwa klabu ya Nkana Red Devils kutoka Zambia imetuma ofa ya milioni 70 za kitanzania kwa ajili ya kumsajili beki Hassan Kessy ambaye mkataba wake na Yanga umeshamalizika.
Kessy ambaye anacheza kama beki wa kulia amemaliza mkataba na Yanga mwezi Mei 2018 na kuwa mchezaji huru ambaye hivi sasa anaweza akafanya mazungumzo na klabu yoyote ile itakayoweza kumsajili.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Meneja wa Kessy, Athuman Tippo, amepokea ofa hiyo kutoka Zambia ambapo timu hiyo imeonesha nia ya dhati ya kumuhitaji mchezaji huyo ambaye Yanga hawajafikia naye makubaliano ya kumuongezea mkataba mwingine.
Tippo amefunguka na kueleza kuwa ni kweli Kessy hana mkataba na Yanga na kinachofanyika hivi sasa ni mazungumzo baina ya klabu na yeye ili kuweza kufikia mwafaka kama ataweza kuelekea Red Devils.
Ikumbukwe Kessy alisajiliwa na Yanga akitokea Simba SC mwaka 2016 na kusaini mkataba wa miaka miwili ambapo sasa inaelezwa Kessy na Yanga wameshindwa kuelewana kuongeza mkataba mwingine kutokana na dau alilolihitaji.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post