PICHA: Yanga safari ya Godson Park Liverpool imemalizwa na Kakamega leo


June 3 2018 mjini Nakuru nchini Kenya mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 yalianza rasmi yakishirikisha timu nane kwa mfumo wa knock Out.

Yanga ambao walienda na kikosi chao kamili nchini Kenya leo walicheza game yao ya kwanza dhidi ya Kakamega Home Boys na kujikuta wakipoteza mchezo huo kwa kipigo cha magoli 3-1.

Kipigo hicho sasa kinaiondoa Yanga katika michuano hiyo na kuifanya Kakamega kuingia hatua ya nusu fainali wakisubiri mshindi wa game kati ya Gor Mahia dhidi ya JKU itakayochezwa muda sio mrefu.

Kipigo hicho sasa pia kinaifanya Yanga kukosa nafasi ya kwenda Godson Park katika jiji la Liverpool kucheza game ya kirafiki dhidi ya Everton kwani Bingwa wa michuano hii atapata zawadi ya fedha kombe na fursa ya kucheza na Everton nchini England.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post