DoneDeal: Kutinyu kaungana na Ngoma Azam
Kiungo wa Singida United Tafadzwa Kutinyu anaungana na kocha Hans van Pluijm kuelekea Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.
Meneja wa Azam FC Philip Alando amethibitisha usajili wa Kutinyu kutoka Singida United.
“Kweli tumememsajili Kutinyu, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine”-Alando
Kutinyu alijiunga na Singida United kabla ya kuanza kwa msimu huu akitokea klabu ya Chicken Inn ya Zimbabwe na baada ya kufanya vizuri ndani ya msimu mmoja akiwa Singida sasa anaelekea Azam.
Akiwa Azam ataungana na raia wenzake wawili kutoka Zimbabwe Bruce Kangwa na Donald Ngoma ambaye pia amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni.