Penzi la Baraka the Prince na Naj laingia Mdudu



Msanii wa bongo fleva ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa kazi yoyote na hapo  awali ali hit na ngoma ya BORA IWE ambaye ni Baraka the Prince, ambae pia amesikika katika ngoma ya Rdj the dj ambayo alikuwa ameshirikishwa na kufanya vizuri amesema kuwa amekaa miezi saba hajatoa wimbo ila anakazi mpya ambayo ataitoa mwezi wa saba na hiyo ni kutokana na mipango yake aliojiwekea asitoe nyimbo hadi mwaka huu mwezi wa saba. 

Vilevile ameongelea kuhusiana na yale yanayoongeleka mitaani kuhusiana na mahusiano yake na Mpenzi wake naj, na hiyo ni baada ya ya Naj kufuta picha za baraka kwenye ukurasa wake wa instagram, ambapo pia baraka aliwahi kumu UNFOLLOW naj kwenye kurasa yake ya instagram ambapo ilizua sintofahamu kwa watu ambapo wengi walihisi mahusiano hayo yamevunjika au la ambapo amesema kuwa hakumu unfollow. 

" Sikumu unfollow Naj tu nili Unfollow watu wote na nikaanza ku follow upya watu ambao nilikuwa nawahitaji kwa muda huo, kwasababu nimekwambia ni baraka mpya kwahiyo nitakapoanza kutoa kazi nitaanza ku follow watu, na mwanzo nili unfollow watu wote wakawa Zero nika follow watu tisa tu na Naj alikuwepo kwenye hao tisa"Baraka Amesema 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post