Wezi wa Instagram Wamkata Kidomo Haji Manara, wameteka Ukurasa wake wa Instagram



Ukurasa wa Instagram wa Afisa Habari  Simba Haji Manara umedukuliwa na wahuni wa mjini na sasa haupo hewani kwa sasa. 

Ukurasa huo wa Manara wenye zaidi ya wafuasi laki mbili umehakiwa na watu wasiojulikana hivyo kuufanya usiendelee kuwepo hewani tangu mapema leo asubuhi.

Muungwana Blog imechimba moja kwa moja kwa Msemaji huyo bila mafanikio na kumpembenyua  mmoja ya wafanyakazi wa klabu hiyo ya simba ambapo alithibitisha taarifa hiyo ya wizi na kupotezwa kabisa kwa akaunti hiyo, amedai tangu siku ya jana jion akaunti hiyo haikuwa hewani ambapo kwa sasa wapo kwenye mikakati ya kumjua mwizi huyo na kuirudisha akaunti hiyo. 

Manara amekuwa akiutumia ukurasa huo kuandika mambo yake binafsi pamoja na kutoa taarifa mbalimbali zinazoihusu klabu ya Simba.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post