“Mechi ilimshinda mwamuzi”-Shaffih Dauda
Tukio la mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kutoa kadi nyekundu kwa Hassan Dilunga halau mchezaji huyo hakutoka limewavuruga watu kibao waliokua wanafatilia mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup vs Singida United.
Mwandembwa alijichanganya wakati anamwonesha kadi ya njano Hassan Dilunga alidhani ni kadi ya pili ya njano kwa mchezaji huyo kisha akamkandamiza na ‘umeme’.
Lakini kumbe ilikuwa ni kadi ya kwanza kwa Dilunga, mwamuzi alijichanga akadhani anatoa kadi kwa Issa Rashid ‘Bada Ubaya’.
“Wakati mwingine waamuzi wanahitaji kuwa na uzoefu ukilinganisha na mechi wanazopangiwa, mwamuzi wa leo mechi ilimshinda.”
“Mara nyingi maamuzi aliyokuwa akiyatoa hakuwa na uhakika nayo, alikuwa kama anabahatisha ndiyo maana tukio la kadi nyekundu linaonesha alipoteza focus.”
“Hakuwa makini ndio maana matukio mengi sana yalikuwa yanamzidi.”