Majeruhi yazidi kukiandama kikosi cha Argentina


Na Elizabeth lyavule.
vijana wa kocha Jorge Sampaoli wameshawasili nchini Urusi tayari kwa michuano ya kombe la dunia huku karata yao ya kwanza wakitegemea kuitupa kukabiliana na timu ya taifa ya Iceland siku ya ijumaa tarehe 16 saa 10 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki.
Wakijawa na matumaini mengi yakubeba kombe la dunia nchini urusi baada ya kupoteza mchezo wa fainali zilizopita dhidi ya Ujerumani kule Brazil, kikosi chao kikiongozwa na Leonel Messi kimezidi kuandamwa na rundo la majeruhi kwa baadhi ya nyota wao muhimu.
Alianza golikipa wao namba moja Sergio Romero aliepata maumivu ya bega katika siku za mwanzo za maandalizi ya fainali hizi za 21 pale Urusi, haikuishia hapo walimpoteza kiungo wao muhimu Manuel Lanzini aliyepata maumivu ya goti siku ya ijumaa hivyo kufanya wote wawili kuzikosa fainali hizo.
Sasa ni zamu ya kiungo mkongwe Eva Bannega ameshindwa kuungana na wenzie kufanya mazoezi kwa siku mbili kutokana na kuwa majeruhi hivyo wanamuangalizia kama ataweza endelea na mashindano haya au safari yake itafika mwisho kuitumikia nchi yake Urusi.
Pamoja na yote macho yao yapo kwa Sergio Kun Aguero kwani hayupo vizuri sana kiafya alimaliza msimu EPL akiwa majeruhi na yalimfanya ashindwe kucheza karibu mzunguko wote wa pili wa EPL.
Japokua wana wachezaji wengi wazuri wanaoitwa kuziba mapengo wanayoyaacha lakini hawatakua na maandalizi kuelekea Urusi kama ya walioumia na huenda ikawa ni mwisho kwa kizazi cha dhahabu walichonacho kutegemewa kuiletea nchi taji lolote.
iwe kopa America au kombe la dunia kwakua wengi wao kama Leonel Messi, Mascherano, Eva Bannega, Kun Aguero na Angel Di Maria wote wanaelekea ukingoni mwa kucheza soka la kiushindani maana wote wana umri juu ya miaka 30 na mashindano haya ni ya mwisho kwa kizazi hichi cha dhahabu kuaminisha wengi kwamba wana uwezo wa kubeba kombe pale Urusi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post