Na Elizabeth Lyavule
Ilianza tarehe 2 February mwaka 1958 ambapo wachezaji wa Manchester United walipata ajali ya ndege na kupoteza maisha. Liverpool walileta kejeli sana baada ya huu msiba mpaka wakaamua kutengeneza nyimbo ya kuwakejeli Manchester United na wakiimba “Your players have turned manure” Wakimaanisha wachezaji wenu waliokufa wamegeuka mbolea.
Watu wanapenda sana kuwakejeli mashabiki wa Manchester United kwa kupitia hili neno “MANURE”Kila mtu anayekejeli Manchester United kwa kupitia hili neno huwa anawakumbusha ajali ya ndege maana chimbuko la hili neno lilianzia huko.
Ilikuwa ni huzuni sana kipindi hicho lakini Liverpool hawakujali waliendelea kushangilia kwa furaha huu msiba. Na kwanini mashabiki wengi wa Manchester United duniani huwa wanaipenda Real Madrid kama timu yao ya pili?
Ni kwa sababu baada ya ajali ya ndege mwaka 1958 mwaka huo huo Real madrid walikuwa mabingwa wa Uefa champions league na waliomba kombe hilo wapewe Manchester United kama kuwafariji na Manchester United walikataa kupewa kitu cha bure ambacho hawajakitolea jasho.
Real madrid hawakuishia hapo wakati ligi imeisha na likizo imeanza waliwaalika Manchester United nchini Hispania na gharama zote waligharamia wao.
Kule nchini Hispania Real madrid waliandaa mechi za kirafiki nyingi tu na waliomba hayo mapato yote wapewe Manchester United ili yawasaidie kujijenga upya.
Real madrid hawakuishia hapo waliamua kumtoa mchezaji wao bora Alfredo De Steffano bure achezee Manchester United. Alfredo De Stefano alikuwa mmoja wa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa Manchester United mpaka wakachukua kombe lao la kwanza la Uefa champion league akiwa anakaribia kustaafu.
Kwa hiyo uhusiano wa Manchester United na Real madrid ni mkubwa na hauwezi kuvunjwa hata kama Ramos angeng’oa bega la Salah fainali ama kumuua Karius.