STRAIKA Mzambia, Obrey Chirwa, amefanikiwa kujiunga na Ismailia
inyoshiriki Ligi Kuu ya Misri kwa mkataba ambao umefanywa kuwa ni wa
siri.
Chirwa ambaye ameitumikia Yanga kwa misimu miwili kabla ya mkataba wake kumalizika hivi karibuni, ametimkia
kwenye timu hiyo kutokana na kushindwana na Yanga katika kuongeza mkataba.
Mzambia huyo alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2016/17, akitokea FC Platinium ya Zimbabwe
kwa ada ya uhamisho wa Sh milioni 240.
Chanzo kutoka Misri kinasema kuwa, mchezaji huyo alikuwa nchini humo
tangu wikiendi iliyopita na juzi Jumatatu alifanikiwa kusaini mkataba.
“Chirwa amejiunga na Ismailia baada ya kuafi kiana makubaliano yao,
hivyo ameachana rasmi na Yanga na sasa atakuwa mchezaji wa timu hiyo
kuanzia sasa,” kilisema chanzo.
Meneja wa mchezaji huyo, Jonas Tiboroha, alipotafutwa hakuweza
kupatikana kulitolea ufafanuzi suala hilo, lakini hivi karibuni alikiri
kwamba Chirwa ameenda Misri kumalizana na moja ya timu ya ligi kuu
nchini humo.
Tags
YANGA