YANGA: TUNAJUA YONDANI ALIPO WANAYANGA TULIENI, HAENDI POPOTE

Baada ya taarifa kuendelea kushika kasi kuhusu beki wa Yanga, Kelvin Yondani kuwa kwenye listi ya wachezaji wanaotaka kuondoka kikosini halo, kuna tamko limetolewa.

Yondani amekuwa akitajwa kuwaniwa na Simba na Azam FC huku mkataba wake ukiwa unaelekea mwishoni wakati huo inaelezwa mkataba wake umemalizika.

Bosi wa Yanga katika sekta ya usajili, Hussein Nyika amesema kuwa taarifa za Yondani kuondooka hazina ukweli kwa kuwa bado ni Mali yao na hawana mpango wa kumuuza wala kumruhusu kuondoka.

"Hizo taarifa za kuwa hajulikani alipo siyo kweli, sisi tunajua alipo na tunawasiliana naye bila tabu," alisema Nyika na kuongeza:

"Yondani bado ni mchezaji wetu, tunawasiliana naye, Wanayanga watulie, wala hajapotea kama inavyosemwa."

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa tata nyingi kuhusu usajili wa wachezaji wa Yanga kuondoka kikosini hapo kutokana na ukata.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post