DEAL DONE, MRISHO NGASA ASAJILIWA YANGA SC.


Uongozi wa Yanga umethibitisha kumsajili mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Mrisho Ngasa ‘Anko’ ambaye alikuwa anachezea Ndanda FC katika msimu uliomalizika hivi karibuni.

Ngasa anarejea Yanga baada ya kumaliza mkataba na Ndanda ya Mtwara.

Muda mfupi kabla kabla dili halijakamilika Ngasa alisema: “Najisikia furaha sana kwa sababu kila ninapokwenda huwa nakumbuka kwamba kuna mchango ambao ninao kwao na wao wanajua.”

Mwenyekiti wa usajili wa jlabu hiyo Hussein Nyika amezungumzia kurejea kwa Ngasa ndani ya Yanga.

“Mashabiki wa Yanga wanampenda sana Ngasa na bahati nzuri hapa ni kwake kwa sababu ana mapenzi na anaonesha wazi kwamba anaipenda Yanga, hajifichi.”

“Msimu huu umekuwa mzuri sana kwa Ngasa ameisaidia sana Ndanda kutoshuka daraja.”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post