Ikiwa bingwa wa VPL 2017/18 ameshakabidhiwa kombe (Simba) vita kubwa kwa sasa kwenye ligi ipo bondeni kwa timu zinazopambana kubaki kwenye ligi kwa msimu ujao.
Majimaji, Ndanda na Njombe Mji ndio zinagombea nafasi moja ya kubaki kwenye ligi, timu mbili kati ya hizo zitashuka daraja kwenda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Je wajua?
Kuna baadhi ya vitu timu hizo tatu zina fanana, kwa pamoja zote zimeshinda mechi nne tu tangu kuanza kwa msimu huu.
Njombe Mji na Majimaji zimeshinda mechi tatu kwenye viwanja vyao vya nyumbani, zikiwa ugenini zimeshinda mechi moja tu.
Ndanda yenyewe imecheza mechi 13 kwenye uwanja wake wa nyumbani (Nangwanda Sijaona, Mtwara) lakini imepata ushindi mara moja katika uwanja huo. Imeshinda mechi tatu kwenye viwanja vya ugenini.
Ushindi wa Ndanda baada ya kucheza mechi 28
- Mbeya City 0-1 Ndanda
- Ndanda 2-1 Lipuli
- Stand United 0-1 Ndanda
- Majimaji 0-1 Ndanda
Ushindi wa Njombe Mji baada ya kucheza mechi 29
- Majimaji 0-1 Njombe Mji
- Njombe Mji 1-0 Kagera Sugar
- Njombe Mji 2-1 Ruvu Shooting
- Njombe Mji 2-1 Ndanda
Ushindi wa Majimaji baada ya kucheza mechi 29
- Majimaji 1-0 Stand United
- Majimaji 2-1 Mbao
- Stand United 1-3 Majimaji
- Majimaji 3-1 Ruvu Shooting
Majimaji na Njombe Mji zenyewe zimeshacheza mechi 29 na kubakiza mchezo mmoja kila timu ili kuhiimisha msimu wa ligi wakati Ndanda tayari imecheza mechi 28 na kubakiwa na michezo miwili ya kuamua hatima yake.
Timu hizo tatu zinatofautiana kwa alama moja moja, Majimaji nina pointi 24, Ndanda 23 na Njombe Mji 22, kimahesabu hakuna timu iliyoshuka daraja hadi sasa kati ya hizo tatu za chini mechi za mwisho ndio zitaamua.