TETESI: MCHEZAJI MWINGINE WA YANGA ASAINI AZAM MIAKA 2


Azam FC inaonekana kuendelea kujiimarisha zaidi katika usajili kwa ajili ya msimu mpya wa 2018-19 kwa kuwa tayari imejipanga kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Taarifa zinaeleza, Azam FC imeanza mazungumzo na beki  pemben wa Yanga Juma Abdul ikitaka atue Chamazi.

Taarifa zinaeleza, beki huyo anaweza kumwaga wino muda wowote kwa kuwa anaonekana amekubaliana na Azam FC.

"Kweli kuna mazungumzo lakini si suala la kulizungumzia kwa kuwa halijakamilika," kilieleza chanzo kutoka Azam FC.

Lakini kutoka ndani ya Yanga, taarifa zilieleza kwamba wanajua kuwa beki huyo ana mazungumzo na Azam FC.

"Tunalijua hilo, lakini sasa hatuna ujanja. Acha tusubiri kwanza kwa kuwa tunajaribu kuwasiliana naye na kujua cha kufanya.

"Kweli tunajaribu kufanya kila kinachowezekana kadiri ya uwezo wetu lakini mambo hayajawa mazuri."

Mambo yameshindwa kuwa wazi kwa kuwa kila klabu imekuwa ikifanya siri suala la usajili kuhofia kupokwa wachezaji na hasa Simba na Azam FC wamekuwa wakichuana sehemu kadhaa katika suala hilo la usajili.

HAKIKISHA UMEINSTALL APP YETU KWENYE SIMU YAKO KAMA BADO HUJAFANYA HIVO BOFYA HAPA

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post