Kiungo aliye katika kiwango bora zaidi wakati huu chipukizi Makka Edward amethibitisha kuwa msimu ujao hatatumia jezi namba nane.
Makka amesema ameridhia kuiacha jezi hiyo ili itumiwe na moja ya majembe mapya yaliyosajiliwa na Yanga.
Makka amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano waliompa katika msimu wake wa kwanza. Ameahidi kufanya mambo makubwa zaidi msimu ujao.
Makka ni miongoni mwa wachezaji wanaokwenda Kenya na kikosi cha Yanga kinachoshiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika amesema Yanga inaendelea na zoezi la usajili kwa umakini mkubwa.
Nyika amesisitiza kwamba hakuna mchezaji atakayeondoka klabuni hapo kama bado wanamuhitaji kwa ajili ya msimu ujao.