RAMOS AICHAFUA HISPANIA


Miaka mine iliyopita Hispania waliwasili Brazil kibabe sana. Wakijua kabisa wao ndio watawala wa soka kwa wakati huo. Kilikuwa kizazi bora cha wahispania. Walikuwa wametoa kutwa ubingwa dunia, Ubingwa wa Ulaya mara mbili 2008 na 2012.
Mchezo wao dhidi ya Uholanzi ilikuwa mchezo wa kisasi hasa baada ya kuwafunga katika mchezo wa fainali kule nchini Afrika Kusini. Goli la Andres Iniesta dakika 4 kabla ya matuta.

Spain walitoka kwa aibu kubwa katika michuano ile dhidi ya Chile ambapo ulikuwa mchezo wao wa lazima kushinda lakini Wachile sio watu wazuri. Hispania wakatolewa ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi. Hivi mnakumbuka lile tukio la Nahodha wa Hispania Iker Casilas akiburuzwa na Roben? Sasa jiulize nahodha wa mabingwa wa Dunia anaburuzwa vile?

Euro 2016 Hispania wakapigwa mabao mawili kwa mtungi na Waitaliano. Huu ulikuwa wakati muafaka kwa Vicente Del Bosque kuachia ngazi baada ya safari ya miaka 8 kama kocha mkuu wa Red furry.

Julien Lopetegui akachukua mikoba ya del Bosque. Chini ya Julien Hispania imeshinda michezo yote 10 ya kufuzu kombe la dunia mwaka huu ikiwemo mchezo wa kulipiza kisasi dhidi ya Italia.

Takwimu za Hispania kwa UjumlaMichuanoMechUshKupDrooUEFA1561012827FIFA KD1761102937Jumla3322115764

Julien hajabadili sana kikosi cha dhahabu cha wahispania ila ameongeza wachezaji wadogo ambao alikuwa nao katika kikosi cha U21. David De gea, Koke, Alcanatara, Dan Carvajal pamoja na Isco Alcaron. Kikosi cha U21 cha Julien kilitwaa ubingwa wa ualaya mwaka 2013.

Safari ya matumaini ya Iniesta

Wakati Edward Lowassa anaondoka CCM aliondoka akiwa na matumaini ya kufanya vyema na chama chake kipya.

Iniesta ameondoka Barcelona lakini bado ana deni la mwisho la kumalizia kabla hajaenda kula pensheni. Zawadi ya goli lake la dakika za mwisho bado linahitajika tena.

Amekuwa mchezaji wa muhimu sana. Ni mchezaji aliyebarikiwa kila aina ya ujuvi uwanjani. Iniesta ni kiungo bora duniani tokea Zidane aondoke kiwanjani. Bila shaka huu ni mchuano wake wa mwisho. Benchi watakuwepo vijana wenye njaa, Isco na Alcantara wote watapigania viatu vya Iniesta.


Licha ya kwamba Iniesta ameanzia benchi michezo mingi lakini bado anahitajika sana.
Takwimu za Iniesta msimu wake wa mwisho

MichuanomechimagolipasiAsistiUefa8 (624)190%2La liga25 (1843)182%2Copa de la rey5––0kirafiki1–––44289%4

Sio kwamba ana msimu mzuri sana lakini uwepo wake uwanjani utatia hamasa kubwa kwa vijana hawa wengie wadogo.

Shida ya Hispania ni ipi?

Kwanza haijawahi kuwa na mshambulaiji bora na wa kuaminika kama Fernando Tores. Pili haiwaji kupata mshambuliaji mweye uwezo nje ya eneo la Hatari kama David Villa.

Takwimu zao mwaka 2009-2010MechiMagoliasistiTores32234Vila45282Jumla77516

Pia washambuliaji hawa walisaidiwa na Pedro Rodruguez ambaye alifunga magoli 52 kwenye michezo 23 msimu wa mwaka 2009 na 2010 na kutengeneza magoli 9.


Msimu wachezaji muhimu waliotwaa nafasi ya Pedro ni Marco Assensio mwenye magoli 11 katika mechi 54. Mwingine ni Rodrigo wa Valencia mwenye magoli 19 katika michezo 44. Hivyo bado kuwa walakini katika safu yao ya ushambuliaji.

Je Julien atatua tatizo hili kivipi?

Njia ni nyepesi tu. Arudie matapishi ya del Bosque.

Wakati Fulani mfumo unaweza kuondoa magepu uwanjani. Mwaka 2016 del Bosque alikumbwa na shida kama hii. Kiwango cha Tores kilishuka sana kiasi kwamba akawa haaminiki tena kuwa mchezaji wa mwisho kuamua matokeo.

Mchezo wa Fainali Del alichezesha mfumo wa namba 9 hewa na akafanikiwa kupata matokeo kwa kuilabua Italia mabao manne kwa nunge. Uzuri ni kwamba Tores huyu huyu aliyeonekana mbovu ndiye aliyetokea benchi na kutandika msumari wa tatu. Kwa mtazamo wangu kwakuwa Hispania imebarikiwa viungo wengi basi mfumo wa namba 9 hewa unaweza kuwasaidia.

Assensio ana uwezo mkubwa wa kufunga hivyo atasaidia kwa kiasi kikubwa kama akiaminiwa. Assensio ana madhara makubwa zaidi kwenye hatua 18 kufikia lango la adui kuliko Isco.

Je kuna uwezekano mwingine?

Inawezekana upo. Ukweli ni kwamba Costa 2014 katika kombe la dunia alivurunda. 2016 mwalimu akamua kusafiri na Nolito pamoja na Morata ambao wote hawa watatazama michuano hii kwenye DSTV.

Kiwango cha Costa sio kibovu sana. Labda tu ni ule ugeni na kutokujiamini lakini huyu nae anaweza akawa msaada mkubwa akisaidiana na Iago Aspas.

CostaAspasMechi2037Magoli725Asisti45Pasi78%78%Nyekundu10

Kwa takwimu hizi bila kupepesa macho Aspas ana haki ya kuanza mbele ya Costa. Shida inakuja kwenye suala la ni nani mwenye uzoefu na ni yupi anaaminika zaidi.

Kundi lao limekaaje?

Wataanza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ureno. Kisha watakutana na vibonde Iran pamoja na Waarabu wa Morroco. Bila shaka hapa tunaona nafasi mbili zitakwenda kwa Ureno na Hispania katika hatua ya 16 bora.

Kwa haraka haraka Hispania anaweza kukutana na mshindi wa kwanza au wapili wa kundi A ambapo linajumuisha timu kama Misri, Uruguay, wenyeji Russia na Mashekh wa Saudia. Hata hivyo kuna uwezekano kati ya Argentine na Ufaransa kukutana na Hispania katika hatua ya kufuzu nusu fainali. Mpo hapo?

Usiyoyajua mengine?U
Sergio Ramos ndiye nahodha wa timu hii. Baada ya Casilas kuachana na soka la kimafaifa sasa mchezaji huyu mtukutu ndiye ataiongoza meli hii.

Na kama Misri watafanikiwa kupita hatua ya 16 na wakapangiwa dhidi ya Hispania itakuwa balaa. Najua unaelewa nachomaanisha. Ramos ndiye mchezaji wa pili aliyeichezea La furia michezo mingi zaidi.

Hii ni kwa mara ya 14 Hispania wanashiriki kombe la dunia. Tayari wameshatwaa ubingwa huo mara moja pekee mwaka 2010. Wakati wanabeba kombe hili la dunia Hispania haikuwa na nahodha mkorofi na mtukutu kamam Ramos.

Ilikuwa na nahodha mpole na mwelewa sana. Mara ya mwisho kufanya vyema katika michuano hiyo ilikuwa mwaka 1950 ambapo walishika nafasi ya 4.

Fahamu pia kwamba, Hispania haijawahi kutoka sare katika michezo 14 ya mwisho ya kombe la dunia. Wamesinda michezo 10 na kufungwa minne.

Wachezaji wageni kabisa

Alvaro Odriozola amepata bahati ya kipekee akiwa na umri wa miaka 22 tu kuitwa katika michuano hii baada ya kufanya vyema na klabu yake ya Real Sociedad. Na wewe usikate tamaa Mungu yupo. Ipo siku nawe utafanikiwa bila kujali upo steji gani.

AlbaMarceloMichezo4844asisti810kuzuia5.13.8Pasi88%84%Magoli35

Nimemfananisha alba na Marcelo ambaye anatajwa kuwa beki mwenye ufanisi mzuri zaidi.

Ubora wa Hispani upo katika safu ya kiungo pamoja na mabeki wa katikati na wa pembeni.

Je Ramos ataipeleka wapi Hispania huku akijua Waarabu na wapenzi wa Mo Salah wanamuombea mabaya? Sitaki kuongekea sana tabia mbaya za Ramos maana kila mtu analijua hilo

Makala hii imeandaliwa Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post