Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameungana na kikosi cha Yanga kitakachoshiriki mashindano ya SPortPesa Super Cup huko Nairobi, Kenya.
Zahera aliondoka jijini Dar es salaam May 19 2018 kwenda DR Congo siku moja baada ya kusaini kandarasi ya kuionoa Yanga.
Kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa pia ana majukumu kwenye benchi la ufunid la timu ya Taifa ya DR Congo akiwa ni kocha msaidizi ambapo May 28 aliiongoza timu hiyo kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Nigeria.
Baada mchezo huo Zahera amerejea kuungana na Yanga ambayo imesafiri jijini Nairobu kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.