NJOMBE MJI YASHUKA DARAJA BAADA YA KIPIGO CHA 3 -0


Ushindi wa Ndanda 3-0  Mwadui umeishusha daraja Njombe Mji ambayo leo haikuwa na ratiba ya mchezo wa ligi kuu, kwa maana hiyo Njombe Mji imeshuka daraja kabla ya mchezo wake wa mwisho.

Njombe Mji ilipanda msimu huu kutoka ligi daraja la kwanza na msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza kutafuta nafasi ya kurudi VPL.

Ikiwa ligi kuu imecheza mechi 29, imeshinda michezo minne, sare 10 huku ikipoteza michezo 15. Imefunga magoli 17 huku ikiwa imefungwa magoli 41.

Miongoni mwa vitu ambavyo Njombe Mji inaweza kujivunia katika msimu huu wa VPL ni kutoa mchezaji mmoja anaewania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kati ya wachezaji 30 ambao wametangazwa kuwania tuzo hiyo.

Njombe Mji itakamilisha ratiba kwa kucheza dhidi ya Mwadui mechi ya mwisho ya msimu huu kwenye uwanja wa Sabasaba-Njombe.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post