Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Kaimu Mkurugenzi wa program ya Mazingira ya Umoja huo, ambapo ofisi zake zipo nchini Kenya.
Kabla ya uteuzi wake Joyce Msuya alikuwa Mshauri wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Asia ya Mashariki na maeneo ya Pacific huko Washington DC.
Ms. Msuya ambaye ameolewa na mama wa watoto wawili, ana elimu ngazi ya uzamili ya Sayansi ya Microbiology na Immunology kutoka chuo kikuu cha Ottawa Canada, na shahada ya Sayansi ya Biochemistry na Immunology kutoka chuo kikuu cha Strathclyde, Scotland.
Joyce Msuya atachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania ambaye alitumikia nafasi hiyo tangu mwaka 2013 na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon.
Tags
kitaifa