HAJI MANARA AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA SIMBA SC.


Afisa habari wa  Simba, Haji Manara amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa kitendo cha kikosi chao kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar mbele ya Rais Magufuli akiwa mgeni rasmi na aliyewakabidhi kombe la ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu wa mwaka 2017/18.

Kupitia mahojiano na chombo cha habari cha Azam Tv, Manara amesema kuwa anawaomba radhi kwakuumizwa na matokeo ya wikiendi hii.

Nitumie fursa hii kuwaomba radhi mashabiki wetu wa Simba ambao waliumizwa na matokeo ya juzi, najua iliumiza sana kufungwa katika ligi kwakuwa watu walitarajia tungemaliza ‘Unbeaten’ lakini ilikera zaidi kufungwa mbele ya Rais Magufuli.

Hata mimi iliniuma sana sijarudi bado katika hali yangu ya kawaida lakini lazima tuchukulie mpira ni mchezo wa matokeo matatu, ilipanwa ligi hii lazima tufungwe tumechukua ubingwa bila kufungwa ila tunamaliza ligi kwa kufungwa kwahiyo tuchukulie ni changamoto tu.

Mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Maji Maji tunaupa uzito kwasababu hatukubali tena kufungwa mechi mbili ijapokuwa tunajua ni timu nzuri, tutakwenda full timu wala hatwendi kidhaifu na tunatarajia mchezo utakuwa mzuri sana na hatwendi kumnusuru mtu kushuka daraja hatuwezi kuuchezea mchezo wa mpira wa miguu.

Mabingwa wapya Simba wanatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Maji Maji huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1 – 0 dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post