MARADHI YABADILI MUONEKANO WA MUIGIZAJI JET-LI


Muigizaji mkongwe kutokea China Li Lianjie ” Jet Li “ ambaye alipata umaarufu zaidi baada ya kufanya movies nyingi Holly Wood inaripotiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo pamoja na ugonjwa unaoshambulia koromeo “Hyperthyroidism”.

Staa huyo kwa sasa anaendelea vizuri kutokana na mujibu wa meneja wake Steven Chasman na kusema kuwa ugonjwa huo wa Hyperthyroidism umekuwa ukimsumbua Jet Li kwa miaka kumi na kwa sasa yupo mjini Tibet , China akipata matibabu.

 

Jet Li ambaye kwa sasa ana miaka 55 amebadilika kimuonekano kutokana na ugonjwa huo unamsumbua kwa muda mrefu na inasemekana pia anashindwa kusimama kutokana na athari za mifupa alizozipata wakati wa kazi yake ya uigizaji .

Jet Li amehusika katika movies mbalimbali zikiwemo Romeo must die, Hero, The Forbidden Kingdom, Kiss of the dragon, The Expendables na nyingine nyingi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post