Moja kati ya habari zilizochukua headlines sana kwa sasa katika soka la Bongo ni pamoja na stori za kocha wa Singida United mholanzi Hans van Pluijm kutangaza kuwa ataondoka club hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Hans van Pluijm ambaye aliwahi kuifundisha club ya Dar es Salaam Young Africans, ametajwa kufikia maamuzi hayo baada ya kudaiwa kuwa amepata nafasi ya kuwa kocha mkuu katika club ya Azam FC ambayo kocha wake Cioba ameripotiwa kutoendelea tena na timu hiyo.
Etienne Ndayiragije
Wakati Hans Van Pluijm akihusishwa kwenda kuifundisha Azam FC, aliyekuwa kocha wa Mbao FC Etienne Ndayiragije ameanza kuhusishwa kuwa mbadala namba moja wa Hans van Pluijm katika club ya Singida United, taarifa zote hizi zinaendelea kuwa tetesi licha ya kuwa Hans ametangaza rasmi kuwa ataondoka Singida.