Baada ya headlines za muda mrefu na maswali yasiokuwa na majibu kuhusiana ni nani atakuwa mbadala wa kocha Arsene Wenger ndani ya Club ya Arsenal baada ya Wenger kutangaza kuwa anaondoka Arsenal.
Leo usiku wa May 23 2018 Unai Emery ametegua kitendawili kuwa yeye ndio kocha mpya wa club ya Arsenal baaada ya Wenger kutokana na ujumbe aliouandika kupitia tovuti yake “Najivunia kuwa sehemu ya familia ya Arsenal”
Kama humfahamu Unai Emery anajiunga na Arsenal baada ya kuondoka katika club ya PSG ya Ufaransa na alikuwa anahusishwa karibu na kujiunga na Arsenal yeye na Mikel Arteta ambaye inaonekana uzoefu umemfanya Emery apate dili hilo.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA