MANARA AFUNGUKA KUHUSU KICHUYA KUITWA KUICHEZEA TP MAZEMBE

Image result for kichuya simba
Hivi karibuni baba mzazi wa Shiza Kichuya alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema, anataka mtoto wake akimaliza mkataba na Simba aende TP Mazembe timu ambayo imeonesha nia ya kutaka kumsajili.
Mkataba wa Kichuya na Simba unaelekea ukingoni lakini baba mzazi wa mchezaji huyo hayupo tayari kuona mtoto wake anasaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Simba baada ya kuonesha kiwango cha juu katika misimu miwili aliyoitumikia klabu hiyo.
Manara akiwa Clouds FM kwenyekipindi cha ‘Leo tena’ ameeleza mpango wa Simba baada ya kauli ya baba yake Kichuya.
“Juzi nikizungumza na Kichuya, baada ya kuambiwa na watu ninaowaamini kwamba mzee wake amezungumza mahali.”
“Kichuya bado anamkataba na Simba lakini ana hamu ya kwenda kucheza mpira nje ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo yake, familia yake, klabu na nchi.”
“Ameniambia kipaumbele chake ni maslahi kwenye mpira kwa hiyo tunajaribu kukaa nae kuzungumza kuona kama ataendelea kucheza Simba lakini akipata nafasi hatutamzuia.”
“Huyu ni kijana wetu amecheza Simba kwa miaka miwili kwa mafanikio, anapendwa sana japokuwa alianzia huko Morogoro, kwa hiyo litakalokuja tutawatangazia lakini ni miongoni mwa wachezaji watakaosafiri kwenda Songea.”


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post