Washambuliaji Lionel Messi, Sergio
Aguero, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain wamejumushwa katika kikosi cha
wachezaji 23 watakaoiwakilisha Argentina kwenye kombe la dunia nchini
Urusi
Lakini mfungaji bora zaidi wa ligi ya Serie A mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi ameachwa nje.Aguero anajiunga na wachezaji wengine watano wa Premier League akiwemo wanayecheza pamoja huko Manchester City Nicolas Otamendi.
- Lionel Messi awafikisha Argentina Kombe la Dunia
- Ni nani mkali zaidi kati ya Lionel Messi, Radamel Falcao, na Alvaro Morata?
- Messi kusalia Barcelona hadi 2021
Nusura watupwe nje ya Kombe la Dunia lakini hat-trick ya mshambuliaji wa Barcelona Messi iliwaokoa wakati wa mechi yao ya mwisho ya kufuzu.
Kikosi kamili cha Argentina
Walinda lango: Sergio Romero (Manchester United), Willy Caballero (Chelsea), Franco Armani (River Plate).Walinzi: Gabriel Mercado (Sevilla), Federico Fazio (Roma), Nicolas Otamendi (Manchester City), Marcos Rojo (Manchester United), Nicolas Taglafico (Ajax), Javier Mascherano (Hebei Fortune), Marcos Acuna (Sporting Lisbon), Cristian Ansaldi (Torino).
Viungo wa kati : Ever Banega (Sevilla), Lucas Biglia (AC Milan), Angel Di Maria, Giovani Lo Celso (wote wa Paris St-Germain), Manuel Lanzini (West Ham), Cristian Pavon (Boca Juniors), Maximiliano Meza (Independiente), Eduardo Salvio (Benfica).
Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain, Paulo Dybala (both Juventus), Sergio Aguero (Manchester City).
Tags
KOMBE LA DUNIA 2018