Msimu uliopita kulikuwa na habari kubwa sana jinsi Diego Costa alivyoondoka Chelsea, mengi yalisemwa lakini kubwa likiwa ni ugomvi na kutokuelewana kati ya Costa na Conte hadi kufikia hatua Conte kumkataa Costa.
Weekend hii nayo kumeibuka story ya namna hii lakini safari hii ni Conte kufanyiziwa na mchezaji mwingine wa Kibrazil, hii ilikuwa saa chache baada ya Chelsea kutwaa kombe la FA dhidi ya Manchester Unite pale Wembley.
Kupitia katika mtandao wa Instagram mchezaji Willian aliweka picha za matukio wakati wakishangilia ubingwa, lakini gumzo kubwa ni baada ya kuifisha sura ya Antonio Conte kwa kutumia emoji za kombe.
Willian hakuonekana na furaha alipokuwa amekaa benchi la Chelsea na wakati pekee ambao alionekana akiwa ana furaha ni pale alipokuwa akiongea na kocha Jose Mourinho wa Manchester United
Tags
MICHEZO KIMATAIFA